GET /api/v0.1/hansard/entries/505798/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 505798,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/505798/?format=api",
    "text_counter": 413,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Gichigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1909,
        "legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
        "slug": "samuel-kamunye-gichigi"
    },
    "content": "Naibu Spika wa Muda, ningetaka kusema kuwa polisi lazima sasa waanze kuangalia hali ya masomo ya wale wananchi ambao wanaajiriwa katika kikosi ya polisi. Haya mambo ya kuwachukua kutoka mahali ambapo wamelelewa na wamesomea na kuwapeleka hapa Kiganjo ama Embakasi na baada ya hapo wanatumwa Baragoi, Lamu na Mandera mahali ambapo kuna vita kabisa, lazima yabadilishwe. Lazima kuwe na sehemu ya mafunzo yao ambayo inawapeleka Baragoi na kule kwa kichaka Mandera ili haya mambo ya ukora ijulikane. Polisi ambao wanatumwa hapo ni wale ambao wameajiriwa hivi juzi. Wale ambao wamekuwa wakikula mshahara na wana uzoevu wa kazi hawatumwi kule kwa sababu wanaweza kuhongana waweze kukaa hapa Nairobi ama sehemu zile ambazo zina usalama. Vijana wetu wa miaka 21 ndio wanatumwa waende kule. Hawa wengine ambao wamepata vitambi hawawezi hata kuenda kufanya kazi hapo. Kwa hivyo, ni muhimu sana mambo ya masomo yabadilishwe. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}