GET /api/v0.1/hansard/entries/506030/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 506030,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/506030/?format=api",
    "text_counter": 119,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Jambo la kwanza nashtumu vikali hao watu wawili kwa kutoa taarifa kama hii kwenye mtandao. Mhe. Hassan, Seneta wa Mombasa ni Seneta ambaye huongea kulingana na fikra zake. Hayuko hapa kuongea ili kumpendeza mtu yeyote. Ni mtu ambaye anaongea vile anavyofikiria na hivyo ndivyo Katiba yetu inavyosema; ya kwamba kuna uhuru wa mtu kusema vile anavyotaka. Jambo la kusikitisha ni kwamba hivi sasa ametishiwa maisha yake. Waswahili wanasema; “Lisemwalo lipo na kama halipo laja.” Kwa hivyo, tishio hili kama halipo hivi sasa, Sen. Hassan amelitubua na ametuambia. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba Bunge la Seneti, kupitia kwako Bw. Spika lichukue hatua ya kutetea maisha ya ndugu yangu Sen. Hassan ili lisemwalo likiwa halipo na laja, tuweze kulikinga lisiweze kumfikia. Nashtumu sana kitendo hiki."
}