GET /api/v0.1/hansard/entries/506031/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 506031,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/506031/?format=api",
    "text_counter": 120,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chelule",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13126,
        "legal_name": "Liza Chelule",
        "slug": "liza-chelule"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika; asante kwa kunipa nafasi hii nizungumze pia kuhusu usalama katika nchi yetu. Nazungumzia mambo ambayo yametendeka siku chache zilizopita. Jambo la kwanza ni yale maafa yaliyotokea Mandera. Pili, ni kitendo cha kuwavua akina mama na wasichana wetu nguo. Tuna hofu sana kama akina mama na wananchi wa Kenya kwa mambo na vitendo vinavyoendelea hapa nchini. Tumeketi hapa kama Maseneta na sisi ni viongozi tunaowaakilisha wananchi pale mashinani. Tuko na Kamati ya Usalama na Maswala ya Kigeni ambayo tumesikia Mwenyekiti akilalamika kuwa mawaidha yake hayatiliwi maanani. Wakati mambo yake hayatiliwi maanani na ilhali ni mwakilishi wetu katika Bunge hili kwa masuala ya usalama, inatushtua sisi kama viongozi. Ninampa pole zangu mwenzetu Sen. Hassan Omar kwa kutishiwa maisha yake. Kama viongozi, Serikali inafaa kuchukua hatua mwafaka. Bw. Spika, tunaposimama hapa tuna mioyo mizito kwa sababu mambo yanayofanyika hapa nchini si mambao ya kawaida. Tuliona jana picha ambayo msichana moja alivuliwa nguo zote. Ingawa wanaowavua akina dada nguo wanasema kwamba wasichana wanavaa nguo fupi, hata unashangaa; kama suruali pia ni fupi. Nguo za juu zinavuliwa hadi chupi. Kwani chupi pia inatikiwa iwe ndefu? Unashangaa ni kwa nini watu wanaendelea kutenda kitendo kama hicho. Sisi kama akina mama na viongozi tunashtumu vikali vitendo hivi. Wasichana wetu jana na leo wanahofia kutoka nyumbani, hawajaenda shule kwa sababu wanahofia maisha yao."
}