GET /api/v0.1/hansard/entries/506129/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 506129,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/506129/?format=api",
"text_counter": 218,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kuunga mkono Hoja hii iliyoletwa hapa na Seneta wa Mandera. Ningependa kusema amani ni kitu cha maaana katika nchi yoyote. Bila amani hatuwezi kuwa na maendeleo yoyote katika nchini. Biashara huimarika kama kama kuna amani. Watalii watazuru nchini ikiwa kuna amani. Uchumi wa nchi yetu hutegemea sana watalii. Vijana wetu wanaweza kufanya biashara ikiwa kuna amani nchini. Jambo la kushangaza ni kwamba hakuna amani katika nchi yetu ya Kenya. Hakuna amani kwa sababu ya mambo tofauti tofauti. Viongozi wakuu waliopewa mamlaka ya kuongoza nchi hii, hasa katika upande wa amani wamezembea kazini. Watu wawili ama watatu katika vitengo vya upelelezi, ujasusi na wanaokabili fujo nchini wamezembea katika kazi zao. Ukiangalia upande wa Lamu utaona kwamba usiku huo kabla ya kisa kutendeka, Gavana alipiga simu na kuzungumza na watu wa Idara ya Ujasusi. Idara ilijua kabisa kwamba Mpeketoni kungekuwa na shida lakini hawakuchukua tahadhari yoyote. Tunauliza kwa nini hakuna jambo lilofanyika kama Idara ya Ujasusi ilipeana habari kwamba kungetokea maafa fulani. Kwa nini watu ambao wamepewa mamlaka ya kushughulika na kuchukua habari kutoka kule hawakuchukua hatua ya kuzuia mambo hayo? Jambo kama hili halifai kuruhusiwa kutendeka katika nchi huru. Kama watu wamepewa mamlaka ya kufanya kazi, basi wafanye kazi. Kama watu hawawezi kufanya kazi, basi wawachie wale ambao wanaweza kufanya kazi. Jambo lingine ambalo linasikitisha sana ni hali ya usalama katika Mkoa wa Pwani kuanzia Kaunti ya Lamu, Kilifi, Mombasa, Kwale, Taita na Tana River. Maeneo haya yote hutegemea shughuli za kiutalii. Sasa hivi, tunaona baadhi ya Misikiti imefungwa. Haya ndio maeneo tulikulia na kusomea. Visingizio vingi vinanza kutokea hapa na pale. Watu wamekuwa wakisema wamepata hiki na kile ndani ya Misikiti. Jawabu si kufunga Misikiti lakini kuwauliza wale ambao tumewapeleka Kiganjo kusoma kujua kwa nini vitendo kama hivi vinafanyika na vile tunavyoweza kuvipinga. Hatufai kukimbilia Misikitini tukisema kuna watu ambao wanafundishwa mambo fulani na wanafaa kushikwa na kuwekwa ndani. Hivi sasa, ukiangalia mahali kama Mombasa au pwani kwa ujumla, kuna vijana wengi ambao wameshikwa. Wamewekwa ndani. Watu wamekuwa wakishikwa kutoka kwa nyumba zao, wanasimamishwa na kuwekwa katika malori na kusafirishwa hadi vituo vya polisi. Watoto, wanawake na vijana wanashikwa bila sababu yo yote. Hatuwezi kuwa na hali kama hii ya sitofahamu. Katiba yetu inasema kushika Mkenya mwingine na kumweka ndani kwa vile unamshuku, huo ni uvunjaji wa sheria. Lazima kuwe na kielelezo fulani ya kwamba mtu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}