GET /api/v0.1/hansard/entries/506131/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 506131,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/506131/?format=api",
    "text_counter": 220,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "fulani ana husika na kitendo fulani ili umshike na kumweka ndani. Hivi sasa, sivyo mambo yanavyoendelea huko Mombasa. Mandera ni mahali ambapo panajulikana. Tuko na ndugu zetu Wasomali na Waethiopia katika Kaunti ya Mandera. Kwa nini mabasi yanayosafiri nje na ndani ya Mandera hayazindikishwe na askari kuwe usiku au mchana? Tunawacha raia waende zao Nairobi bila kujali usalama wao. Hiyo ni hatua ndefu. Lazima kuwe na mipango ambayo itafanywa kisawasawa ili wawe na usalama wakisafiri nje na ndani ya Mandera. Usalama wao wanaposafiri unafaa kuwa umehakikishiwa na Serikali. Jambo la kusisitiza ni kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa pwani ni utalii. Watu wetu wa Taita Taveta, Mombasa, Kilifi, Kwale na Tana River hutegemea utalii. Wakati huu, hakuna mtalii ambaye anazuru mbuga za wanyama kama vile Tsavo National Park. Mahoteli yote yamefungwa. Taita kuna mahoteli karibu ishirini na yote yamefungwa. Ukija Mkoa wa Pwani kuanzia Lamu hadi Lunga Lunga, utaona mahoteli mengi yamefungwa. Watu wataendelea kuishi vipi? Kulingana na Katiba, usalama wa nchi uko mikononi mwa Rais. Rais wetu ataingia katika kumbukumbu za historia kama hatachukua hatua. Yeye si Rais peke yake lakini pia Amri Jesi Mkuu wa Majeshi yote ya Kenya. Lazima achukue kiboko sasa na kuwafuta watu kazi ambao wamezembea. Nakubaliana sana na Hoja hii ya kwamba Rais ana mamlaka ya kuangalia na kuona ni nani ambaye amezembea na kuchukua hatua mwafaka. Rais wetu akiwa hatachukua hatua, hilo litakuwa kosa kwa vile ana mamlaka ambayo amepewa na wananchi 40 milioni. Ningependa kusema kinaga ubaga. Hatufai kuficha jambo lolote ikiwa baadhi ya Wakenya wamepoteza maisha yao. Kama Bw. Kimaiyo hawezi kufanya kazi yake, basi Wakenya wamechoka naye na litakuwa jambo la busara ikiwa atang’atuka cheoni chake ili Rais amchague mtu mwingine ambaye itaimarisha usalama wetu."
}