GET /api/v0.1/hansard/entries/506133/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 506133,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/506133/?format=api",
    "text_counter": 222,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, pia ikiwa Bw. ole Lenku ameshindwa kuyazingatia mambo ya usalama, basi ni lazima ang’atuke mamlakani ili ampe nafasi Rais amchague mtu mwingine ili aimarishe usalama hapa nchini. Huyo mtu mwingine ataiendesha dao la usalama na wananchi watakuwa na imani naye. Hivi sasa, Wakenya hawana imani kabisa na watu hawa wawili. Ni lazima Rais aliyechaguliwa na Wakenya na ambaye yuko katika mamlaka sasa kama Rais wa Jamhuri ya Kenya na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi na kuambatana na Katiba hawafute kazi hawa watu wawili na kuteua wengine ambao watafanya kazi vizuri. Wakenya wanafaa kulala katika nyumba zao wakijua kuna amani. Watu wa pwani ni watu wa amani. Hivi leo ukiangalia, watu wanaenda Disemba kwa likizo. Zamani wakati kama huu Mkoa wa Pwani ulikuwa na watu wengi sana, hasa watalii. Hata watu wetu wa kutoka bara ama kutoka nchi za huku juu walikuwa wanakuja kule kwa sababu ni mahali pa kustarehe. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}