GET /api/v0.1/hansard/entries/506517/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 506517,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/506517/?format=api",
    "text_counter": 330,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwashetani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2163,
        "legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
        "slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
    },
    "content": "Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Usalama umekuwa suala gumu. Ni suala ambalo bila vitengo vya usalama kukaa sawasawa na kubuni mipango mipya ambayo itaweza kuboresha usalama, tutakuwa kati ya wale wanaopata hasara. Ninapozungumuzia haya, ninatoa mfano wa kitegauchumi kule kwetu Kwale. Pwani, kwa jumla,tumekuwa katika hali yakutoelewa kwa nini uchumi wetu unashuka. Ukiangalia sekta ya utalii, kati ya wale wanaofaidika ni sisi watu wa Pwani. Sasa hivi, asilimia themanini ya wale ambao walikuwa wakifanya kazi kwenye hoteli hawana kazi. Kina mama ambao walikuwa wakishona viondo na vijana ambao walikuwa na lugha tofauti ya kujieleza kupitia kwa watalii, wote wamekosa kazi. Kwa hivyo, ni suala ambalo mpaka sasa, hatujui ni mipango gani Serikali imetuwekea ili kuhakikisha utalii umerudi jinsi ulivyokuwa zamani. Pia, ukiangalia tatizo lililopo ni rasilimali zetu za Pwani kushuka bei. Ukiangalia nyumba ambazo watu walikuwa wakilipa Kshs.30,000 ili waishi, kwa sasa hata ukiuliza Kshs.5,000 huwezi kupata. Usalama umechangia watu wa Pwani kutofaidika kiuchumi. Vile vile, ukiangalia usalama, sasa hivi nchi nzima kuna matatizo ya usalama. Kwa mfano, juzi watu waliuliwa kule Mandera. Pwani kumekuwa na suala hili kwa muda mrefu. Viongozi wetu wakidini wamekuwa wakiuawa mmoja mmoja bila sisi viongozi kuletewa ripoti ya sababu za viongozi hao kuuliwa. Hadi leo, hatujapata sababu wala wale waliohusika katika mipango hiyo. Hatujaambiwa kuwa wameshikwa. Ni suala ambalo limesababishwa na mambo mengi. Mojawapo ya sababu zilozofanya usalama kudorora ni ajira, kama vile alivyotanguliza Rais katika Ripoti yake. Suala la ajira ni suala ambalo lina changamoto kubwa. Sisi wananchi wa Pwani tumelia na kuzungumza kuhusu sehemu ambayo ilikuwa ikiwasaidia vijana wetu kupata ajira. Hizi ni sehemu kama Halmashuhuri ya Bandari ya Mombasa (KPA). Shirika hili ni la awali kabla uongozi huu haujaingia. Ni shirika ambalo lilikuwa linapeana kazi kwa vijana. Kazi hizo zilikuwa zikiwasaidia kuwapa mapato na chakula katika maisha yao. Lakini kwa sasa hivi, miaka karibu saba imepita hakujaajiriwa vijana. Hili ni suala ambalo tumelizungumzia sana lakini mpaka leo hatujapata suluhusho. Ndiposa sisi viongozi wa Pwani tunasema hizi Halmashauri zirejeshwe kwa kaunti ili tuziendeshe wenyewe na zitufaidishe kama wakazi wa sehemu hizo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}