GET /api/v0.1/hansard/entries/506625/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 506625,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/506625/?format=api",
"text_counter": 438,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ramadhani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2388,
"legal_name": "Suleiman Dori Ramadhani",
"slug": "suleiman-dori-ramadhani"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimesimama ili kuchangia suala la usalama. Mwanzo natuma risala za rambirambi kwa familia zilizoathirika na mambo ya usalama. Ni jukumu letu sisi Wabunge kuangalia mambo muhimu ya usalama na kuyaelekeza kwa wananchi wetu. Kwa hakika, wakati umefika kwa Bunge hili kuacha maslahi ya kisiasa ambayo yametanda na kuangalia maslahi ya nchi hii. Ni jukumu letu sisi viongozi kuhakikisha tumelinda usalama wa nchi hii. Kama tunavyojua, Bunge lina kazi tatu; ya kwanza ni kuwakilisha, ya pili ni kutunga sheria na ya tatu ni kuwa macho ya Serikali. Suala la usalama limetatiza. Kila wiki tunakuja Bungeni humu kuzungumzia suala la usalama. Kuna suala ambalo lazima tujiulize kama viongozi. Ikiwa tuna majukumu matatu ya kushughulikia, ni kitu gani kinatuzuia kutoa suluhisho la nchi hii kuhusu usalama? Serikali ina jukumu la kuhakikisha kwamba waathiriwa wote wana haki ya kulindwa. Kwa mfano, kuna sehemu zilizoathirika kama vile Kapedo, Mpeketoni, Wajir, Moyale, Kwale, Garissa na Mombasa. Wizara inayohusika imechukua hatua gani ya kuketi na viongozi, kutoa mwelekeo na kupata suluhisho kwa waathiriwa wote ambao hawajapata kitu chochote kutoka kwa Serikali kwa miezi sita au saba? Wizara lazima ijue majukumu yake. Ikijua majukumu yake, nina hakika kwamba suala hili la usalama litakuwa si suala la watu kuelekezana vidole. Kama wizara haitafanya majukumu yake, lazima ishutumiwe. Ndio maana tunasema kwamba ole Lenku, Kimaiyo na mwingine yeyote anayehusika na kudorora kwa usalama katika nchi yetu ya Kenya, lazima apumzishwe na tulete njia nyingine ya kuboresha usalama. Kuna mambo ambayo ni lazima tuyaangalie. Hali ya uchumi katika nchi yetu imedorora sana. Nikiwa katika upinzani na wale wenzetu ambao wako katika upande wa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}