GET /api/v0.1/hansard/entries/506626/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 506626,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/506626/?format=api",
    "text_counter": 439,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ramadhani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2388,
        "legal_name": "Suleiman Dori Ramadhani",
        "slug": "suleiman-dori-ramadhani"
    },
    "content": "walio wengi, tunasema kwamba, ikiwa suluhisho ni majopo haya mawili yaungane ili nchi yetu itapate uokozi, tuko tayari kuungana. Lakini tusichukue suala la makosa ya wale walio kwenye uongozi tukaanza kulaumu upande ambao hauwezi kufanya lolote. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ni jukumu letu, kama viongozi, kuhakikisha tumelinda Wakenya. Tusije hapa kila wiki ikawa tunazungumzia mambo ambayo hayaleti mwelekeo wowote kwa Wakenya. Wakenya wametuchagua. Wakenya wana imani na viongozi na ni lazima tuwatendee kazi Wakenya. Misikiti ambayo imefungwa, nyumba za maombi ni nyumba ambazo ni lazima zipatiwe heshima. Ni nyumba dini zote mbili zinaamini ni nyumba takatifu. Kwa hivyo, tusiingize mambo ambayo hayahusiki kuingizwa katika nyumba zetu za ibada. Ni jukumu letu kama viongozi kusimama kidete kuhakikisha tumelinda nyumba takatifu, nyumba za maombi. Kwa hivyo, ombi langu ni Serikali miliki ama Serikali ya Mhe. Rais Uhuru ihakikishe imeangazia vyema suala la usalama---"
}