GET /api/v0.1/hansard/entries/507787/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 507787,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/507787/?format=api",
"text_counter": 246,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mhe. Spika, unakumbuka kuwa haya mambo yalitokea Shirika la Reli la Kenya lilipopeanwa kwa kampuni na kusemekana kuwa kampuni hiyo itaendesha Shirika la Reli lakini ikawa haina ujuzi wala mwelekeo. Mpaka hivi sasa tunaposema, hakuna mabehewa yamenunuliwa. Hamna chochote kimetendeka kwa Shirika la Reli. Kwa hivyo Mhe. Spika, hii ni moja tu ya Ripoti zilizoko na zilizotakikana kuangaliwa na Bunge la Kumi ama Bunge la muhula ule uliopita. Kamati husika haikuweza kuziangalia na ndio maana imebidi Kamati hii iende mbele sana na kuhakikisha kuwa Ripoti zote zimemalizika na kuletwa kwako ama kwa Bunge ili Bunge liziangalie na kuzipitisha. Hii ni kwa sababu Ripoti kama hii inahusisha mashirika kadha wa kadha na ni mengi. Ripoti hii ina mashirika 20 na vile mwenzangu amesema, labda haoni ni vipi Kamati hii ingeweza kuziangalia. Hata hivyo na kama ujuavyo Mhe. Spika, tumechukua muda na kuomba ruhusa yako ya kipekee ili Kamati hii ipate kuchunguza Ripoti hizi zote. Kazi ambayo imefanywa na Kamati hii, Mhe. Spika inaridhisha na ni ombi langu kuwa Bunge lipitishe na kukubali Ripoti hii ambayo imepeanwa na Kamati ya Bunge kuhusu Uwekezaji wa Umma. Kwa haya machache, naomba niunge mkono Ripoti ambayo tumeipeana hapa. Naweka tamati, Mhe. Spika."
}