GET /api/v0.1/hansard/entries/510112/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 510112,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/510112/?format=api",
    "text_counter": 137,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Gichigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1909,
        "legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
        "slug": "samuel-kamunye-gichigi"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono huu mjadala na Mswada ambao mhe. Lekuton ametuletea. Huu Mswada umeletwa wakati muhimu na unanihusu kwa sababu mwaka jana, niliwapoteza wanafunzi wanne wa St. Peters katika eneo langu la Bunge la Kipipiri. Wanafunzi hao waligongwa na gari ambalo lilikuwa linaenda kwa kasi sana na likatoka barabarani na likawakuta kando ya barabara na wakafariki. Ulikuwa ni wakati wa majonzi sana. Katika mwaka huu pia, tumewapoteza mwanafunzi wengine wawili kule Manunga. Kwa hivyo, sheria hii itakuwa muhimu sana kuhakikisha kuwa watoto wetu hawauawi, haswa kwenye barabara za lami ambapo magari huenda kwa mwendo wa kasi. Baada ya ajali kufanyika, wananchi hukimbia kuweka ilani na vizuio kuonyesha kuna ajali, ilhali kila mmoja wetu anajua kuwa karibu na shule, watoto huvuka barabara mara kwa mara na kuna uwezekano wa ajali kufanyika. Kawaida, wananchi hukimbia kama farasi kutoka zizini. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}