GET /api/v0.1/hansard/entries/510113/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 510113,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/510113/?format=api",
"text_counter": 138,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Gichigi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1909,
"legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
"slug": "samuel-kamunye-gichigi"
},
"content": "Nimeangalia sheria hii na inasema kuwa mahali popote ambapo kuna shule au kituo cha afya, madereva wasizidishe kilomita 30 kwa saa. Pia, wanaohusika na barabara waweke ilani na ishara kuwajulisha madereva kuwa kuna shule au kituo cha afya. Pia, ilani hizi zitaonyesha kiwango cha mwendo ambao madereva wanafaa kuendesha magari yao. Shida ambayo tuko nayo ni kuwa kila wakati, hizo ishara na tarifa zinawekwa lakini wezi wa vyuma wanazing’oa. Madereva wanashindwa kujua ni wapi kuna shule karibu. Katika sehemu ya pili ya sheria hii ambayo Mhe. Lekuton amependekeza iwe hatia kwa madereva, ningeomba tuseme kuwa ni hatia kupitisha kiwango cha mbio ambacho kimewekwa. Pili, sheria inafaa kuyapatia jukumu mashirika yote ya barabara. Mashirika yote ya barabara yanafaa kuwa na jukumu hili. Siyo kwenye barabara kuu peke yake ambapo kuna shule na vituo vya afya. Hata kando ya barabara ndogo ndogo kuna mashule na vituo vya afya na mashirika ya barabara yanastahili kupewa jukumu la kuweka ilani ya kuonyesha kuwepo kwa shule au kituo cha afya. Ningependekeza kuwe na mabadiliko machache katika sheria hii ambayo imependekezwa. Tunafaa kuyapatia mashule jukumu la kuhakikisha kuwa kuna watu mlangoni mwa shule kuwasaidia watoto kuvuka barabara. Wenzangu wamesema kuwa kuna mashule ambayo yamewaajiri watu ambao wanainua ishara ya kusimamisha magari ili wanafunzi wavuke barabara. Ni muhimu tuliweke jukumu hilo kwa upande wa shule au Serikali. Sisi kama viongozi na mashirika ambayo yanahusika, tunafaa kuweka daraja za miguu mahali popote ambapo pana shule, ili badala ya watoto kuwa wanakimbia kila wakati, wanatumia daraja hizo. Huenda tusiwe na peza za kutosha kuweka daraja kila mahali, lakini tunafaa kuweka daraja za miguu ili watoto watumie kuvuka barabara. Wenzangu wameongea kuhusu waendeshaji baskeli na pikipiki. Tumehakikisha kuwa wote wamepata mafunzo ya uendeshaji wa boda boda na wamepata leseni. Ni muhimu tuwe na mradi wa kitaifa kuhakikisha vijana wetu ambao pia wanachangia uchumi na wamepata ajira kupitia kwa piki piki, wamepata hayo mafunzo ili waache kubeba wateja wengi na kuendesha piki piki kiholela holela. Inasikitisha kuona magari ambayo yanawabeba wanafunzi yakiwa katika hali mbaya. Hata katika mashule mapya, magari ni makuukuu. Yamezeeka na wakati wote yanaweza kuharibikia kwa barabara. Ningeomba sheria hii ihakikishe kwamba magari ambayo yanawabeba wanafunzi yako katika hali nzuri, sio kwa viti peke yake. Maafisa wa trafiki, wengi wao ambao wameharibu jina la polisi kwa jumla kwa sababu ya kuchukua hongo, wawe wakihakikisha kuwa magari hayo yako katika hali nzuri. Maafa mengi ambayo yanatokea katika nchi hii hayasababishwi na madereva peke yao, bali maofisa wa trafiki wanawachilia magari ambayo hayafai kabisa kuendeshwa katika barabara zetu. Pia, watu ambao wanatembea barabarani, wanafaa kuangalia maslahi yao na usalama wao. Hawafai kuvuka barabara kabla ya kuangalia kama kuna magari yanapita. Hapa nchini, madereva hawaheshimu wanaotembea. Katika nchi zingine, watu wakivuka barabara, magari yanasimama hata kama hakuna kivukio cha miguu. Kwa hivyo, wao pia wawe waangalifu. Nikimaliza, wazazi na walimu pia wako na jukumu la kuhakikisha kuwa wanafunzi wana usalama katika barabara. Inasikitisha sana kuona asubuhi mtoto aliye na miaka minne au mitatu akiwa amebebwa na mwingine ambaye yuko na miaka mitano wakienda shule. Wamemuacha mzazi kwa nyumba ama wanatoka shule na wamewaacha The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}