GET /api/v0.1/hansard/entries/510115/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 510115,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/510115/?format=api",
    "text_counter": 140,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Chea",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1694,
        "legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
        "slug": "mwinga-gunga-chea"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, ningependa kuichukua fursa hii kukushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Mswada huu. Nitaanza kwa kumshukuru Mhe. Lekuton ambaye kwa wazo lake la burasa, ameuleta Mswada huu. Mswada huu unaelekea hasa kuangalia maswala ya usalama wa watoto wa shule. Ukiangalia baadhi ya mambo ambayo yamezungumziwa, Mswada huu unaangalia usalama wa baadhi ya watumiaji wa mahala tofauti tofauti Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, haswa ukiangalia Mswada wenyewe, unahimiza kuweko kwa baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kutusaidia kupunguza maswala ya ajali. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, Mswada huu ukiwa utapita - na ni matumaini yangu kwamba utapita - utaweza kutusaidia sisi kwanza kama wakaazi wa Kaloleni. Ukiangalia katika eneo ambalo ninawakilisha, bali tu na zile barabara zingine, kuna barabara mbili muhimu. Ya kwanza ikiwa ni ile ya kutoka maeneo ya Mariakani kuelekea Kaloleni ambapo karibu shule tano ziko karibu na barabara. Barabara hii ni muhimu sana kwa sababu inatumiwa na magari mengine ambayo hayawezi kuenda Mombasa ili kuepuka msongamano wa magari. Ukiangalia pia kuna baadhi ya makampuni ambayo yamejenga na yana magari makubwa sana. Tena kuna shule na ajali pia zimekuwa nyingi sana. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, kwa hivyo ningependa kusema kwamba Mswada huu ni muhimu sana. Kuna baadhi ya mambo ambayo lazima tuyaangalie. Jambo la kwanza ambalo lazima tutazame ni mafunzo ya madereva. Utakuta kwamba asilimia 90 ya zile shule ambazo ni za kufundisha watu wetu jinsi ya kupeleka magari, yameandika kwa lugha ya Kimombo “ guaranteed pass.” Hii ni kuonyesha kwamba katika shule hizo, hakuna hata mtu moja ambayo ataanguka mtihani wa kuendesha gari. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, pia ukiangalia sana utakuta kwamba kitu ambacho kinahitajika kwa mtu kuweza kupeleka gari ni kitambulisho chake cha kitaifa. Hakuna maswala ya kiwango cha elimu; ni kitambulisho cha taifa peke yake kinachohitajika. Unaanza kusoma na baada ya wiki tatu, umehitimu kuwa dereva. Cha kushangaza ni kwamba hakuna nafasi ya watu kuweza kupewa mafunzo mara kwa mara ndio waweze kukumbushwa baadhi ya yale mambo ambayo waliyasoma wakiwa shule. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, kwa hivyo, nasisitiza kwamba tukiangalia marekebisho ambayo yatafanywa kwa hiyo sheria ya trafiki, ni muhimu pia kuangalia maswala ya mafunzo ya madereva. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, jambo lingine ambalo ningependa pia kuliangazia ni kuhusu wale ambao wanahusika ama washikadau katika maswala ya trafiki. Kuna baadhi ya madereva ambao leo hii wanapeleka magari katika barabara zetu na baadhi yao labda kwa kupitia amri za mahakama, walipigwa marufuku miaka kadhaa kupeleka magari. Leo, watu hao wamepata zile tunaita copy za zile leseni zao na wako kwa barabara zetu na wanapeleka magari na watu hawajali. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, kwa hivyo, kuna haja ya kwamba wale ambao wanahusika, haswa askari wanaohusika katika maswala ya trafiki, waangalie The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}