GET /api/v0.1/hansard/entries/510116/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 510116,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/510116/?format=api",
    "text_counter": 141,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Chea",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1694,
        "legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
        "slug": "mwinga-gunga-chea"
    },
    "content": "swala hili. Katika kuangalia ulinzi wa watoto wetu shuleni, haswa kwa magari ya shule, ni muhimu pia zile shule ambazo huajiri madereva zikae chini na kukagua stakabadhi zao. Sio eti kwa sababu mimi nikiwa Mheshimiwa ama labda mwalimu mkuu wa shule amefanya mpango akapata gari, basi mtu yeyote anaweza kuajiriwa kuwa dereva, hivyo sio vizuri. Ni lazima kamati ambayo inahusika na mahojiano wahusishe idara inayohusika na usafiri ili wakague madereva hao. Wafanyiwe mtihani vizuri kabla ya kuruhusiwa kuendsha watoto wetu. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, ikiwa mambo haya yote yataweza kuzingatiwa, utaona kwamba usalama wa watoto wetu kwa usafiri utaimarika. Kwa hayo maneno mengi, ningependa kuunga mkono Mswada huu."
}