GET /api/v0.1/hansard/entries/510132/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 510132,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/510132/?format=api",
"text_counter": 157,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadime",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, nashukuru kwa fursa hii. Naamka kuunga mkono Mswada huu. Kwa kweli, kudhibiti mwendo wa kasi kwa magari ni jambo mwafaka kabisa maanake ajali nchini mwetu zimekuwa nyingi mno. Ukiangalia ulimwengu mzima, kwa sasa hivi tuko nambari 22 kwa nchi zenye ajali nyingi ilihali tukiangalia idadi yetu yote ni watu kama 40 milioni na China ina watu zaidi ya 1.5 bilioni lakini ajali zao ni kidogo sana. Nampongeza hon. Lekuton kwa kuleta huu Mswada na ingekuwa vyema pia katika shule zetu na taasisi za Serikali waweke matatu kwa barabara ambazo zinaweza kudhibiti mwendo wa kasi. Vile vile wangeweka vivukio kwa shule zetu hasa za msingi maanake ajali hapa nchini zimeongezeka sana. Watu wengi wamechangia huu Mswada na ninaona yale waliochangia yanaambatana na singependelea kuyarejelea. Nasimama tena kuunga mkono huu Mswada."
}