GET /api/v0.1/hansard/entries/510138/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 510138,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/510138/?format=api",
"text_counter": 163,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Asante sana, Madam. Spika. Nasimama kuunga mkono huu Mswada. Kwanza ninampongeza Mhe. mwenzetu kwa kutuletea huu mjadala ulio wa maana sana katika taifa hili letu, maana ni wa kuokoa maisha. Tukiwa tunachangia huu mjadala, ni lazima tuangalia na pia tujiulize hata hizi ajali zikitokea, kuna shida gani? Haswa ningezungumzia kuhusu ujenzi wetu wa barabara. Ukiangalia barabara zetu, hazina sehemu zimetengwa hususan kwa watu wanaotumia pikipiki. Ningeomba Wizara inayohusika, tunavyoendelea na ujenzi mpya wa barabara zetu au ukarabati, waweze kutilia maanani ili tuweze kuwa na sehemu ambazo waendeshaji boda boda wataweza kuzitumia. Naibu Spika wa Muda, kuna matuta mengi yaliyo katika barabara zetu lakini huwezi kuyatambua maana hayatambuliki. Yanastahili kuwa na rangi maalum ambayo, ukiwa mbali unaweza kujua, pale kweli pana tuta ili uweze kupunguza mwendo. Katika The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}