GET /api/v0.1/hansard/entries/510139/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 510139,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/510139/?format=api",
"text_counter": 164,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "hali hiyo, unakuta ajali zinatokea maana, mtu atakuja kwa kasi bila kujua kwamba, pale kuna tuta na mwishowe gari lake linatatisika ama kuvunjika. Katika huu ujenzi wa barabara, katika sehemu zetu za mashambani, utashangaa ya kwamba, upana wa barabara ni ule ule tangu wakati wa ukoloni ambapo, pengine ni gari moja tu lililokuwa linapita katika barabara hiyo. Barabara hiyo ni nyembamba sana. Wakati wa mvua, inakuwa mbaya zaidi maana, barabara yenyewe vile ilivyolimwa, ina mavumbi hapo katikati. Gari linapaswa kupita katikati ya ile barabara. Likitokea gari lingine ama pikipiki, kupishana ni vigumu. Mwisho unaingia ndani ya mtaro ama mgongane. Tunaomba ujenzi wa barabara uangaliwe zaidi. Pia, tukizungumzia mifereji ya kutoa maji machafu kwa barabara, ninashangaa hao waandisi wetu kule nyanjani wanafanya kazi gani; haswa katika Kaunti ya Kwale. Utapata kwamba anayeweka mfreji wa maji machafu barabarani anafanya kazi duni sana. Anauweka huo mfreji juu sana kiwango kwamba gari likipita katika hiyo barabara linauvunja. Ule mkorogo wa simiti uliowekwa pale uko juu ya ile barabara kiwango cha kwamba, anayekuja na gari lake, hata kama haji kwa mwendo wa kasi, gari lake litavunjikia pale palipokuwa na ule mfreji. Hii ni kwa sababu huo mfreji haukuwekwa na ujuzi ila tu, uliwekwa ili watu wapate pesa. Kuna ufisadi mwingi sana katika ujenzi wa barabara ambao pia unachangia katika kusababisha ajali. Kwa upande wa boda boda, ni ombi langu kwa Serikali Kuu ione kwamba, wale wanaofunza madereva wetu wa pikipiki, waweze kurudishwa katika maeneo yetu ya makaunti, ili vijana wetu waweze kusomeshwa ama kuenda katika vituo vya mafunzo wakiwa karibu, kwa maana hawana pesa na wanaitaka ile kazi ya boda boda. Lakini kwa sababu kuna mahali huduma ya boda boda inahitajika wakubaliwe kuendesha pikipiki. Kwa mfano, kwetu sisi kule Kwale Kaunti, inamlazimu mtu aende Mombasa. Inabidi, wale vijana wajifundishe vichochoroni na mwishowe wanachukua pikipiki na wanasababisha ajali kwa sababu hawajui sheria za barabarani."
}