GET /api/v0.1/hansard/entries/511139/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 511139,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/511139/?format=api",
    "text_counter": 279,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Gichigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1909,
        "legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
        "slug": "samuel-kamunye-gichigi"
    },
    "content": "Mhe. Spika, nitaomba uniongezee dakika mbili ambazo zimepotea hapo. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu. Huu ni wakati wa kushughulikia mambo ya usalama. Miezi kadhaa iliyopika, kunashambulizi ambalo lilitokea kwa matatu katika Barabara ya Thika na miongoni mwa waliokufa ni kijana mmoja aliyekuwa ametoka kwangu. Alikuwa na mke wake ambaye aliumia miguu mpaka sasa hivi, hawezi kutembea. Kila siku anaenda hospitali na imetubidi kurudi kwa mifuko yetu ili tumchangie. Amewachwa mjane na mlemavu kwa wakati huu. Juzi, tulihudhuria mazishi ya dada huko Kieni ambao waliuawa. Ungekuwa miongoni mwa wale waliohudhuria hayo mazishi, haungejaribu kuzipinga sheria hizi. Miezi kadhaa iliyopita, Kiongozi wa Upinzani alisema kuwa anataka kuwe na majadiliano kuhusu usalama."
}