GET /api/v0.1/hansard/entries/511287/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 511287,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/511287/?format=api",
    "text_counter": 427,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2715,
        "legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
        "slug": "esther-nyambura-gathogo"
    },
    "content": "Ahsante sana Mhe. Spika kwa kunipa hii nafasi ambayo nimengojea sana. Kwanza, ningetaka kushukuru sana kwa mwaka ambao tumekuwa nao. Nataka kukushukuru Mhe. Spika kwa sababu umekuwa na sisi na umetuelekeza kwa njia nzuri. Nataka tena kumshukuru Katibu wa chama cha ODM ambaye alichaguliwa juzi. Ashikane na Serikali ndio tuweze kulisadia na kulijenga taifa hili la Kenya. Hata Mwenyekiti naye namshukuru sana. Mhe. Spika, kuna mambo mawili au matatu ya muhimu ambayo ningependa kuyasema. Mimi niko katika Kamati ya CDF na tumejaribu sana. Wabunge ambao wako katika maeneo yao ya bunge siku hizi hawateti sana kwa sababu tumejaribu sana. Mimi na Mwenyekiti tutahakikisha ya kwamba kila Mbunge ako na pesa zake na anazitumia. Ningependa kuwaambia kwamba ukiwa na Kshs10 milioni katika akaunti yako ya CDF, hakuna vile utapata pesa zingine. Kwa hivyo, wale walikuwa wanauliza ni kwa nini hawajapewa pesa zao, waangalie katika akaunti zao. Meneja wa fedha wako ndiye anaweza kujua ni kwa nini hauna pesa. Tuko na mambo mengi ambayo tutafanya. Mhe. Spika, ningependa kusema jambo moja, ya kwamba tunaelekea katika msimu wa Krismasi. Tukumbuke kwenda na kusherehekea na wale ambao wako chini. Kuna wale ambao hawajui ni nini kinaendelea kwa sababu wako chini sana katika maisha. Tuangalie wale ambao hawawezi kuwekelea hata sahani moja ya chakula katika meza zao. Mimi ningetaka kuomba waheshimiwa wenzangu hivi: Ukikaribia Ruiru hata hautalipa pesa ya kuja! Hata ukikosa gari, unaweza kuja kwa miguu ili tusherehekee pamoja. Watu wangu wa Ruiru ni wakarimu sana. Tena, Ruiru ni hapa karibu. Nahuzunika sana kwa sababu tunaelekea Krismasi na wale ambao wako kwa maofisi yetu bado hawajapokea mishahara yao na wengine wanalia. Wengine wamefungiwa manyumba na wengine hawana----"
}