GET /api/v0.1/hansard/entries/511313/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 511313,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/511313/?format=api",
"text_counter": 453,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii kuunga mkono wenzangu na kuzungumzia suala hili la kuelekea likizoni. Mwaka huu ulikuwa mgumu sana kwa sababu Wakenya wengi sana wameuawa bila sababu; ni kama ilikuwa kitubio. Lakini Mwenyezi Mungu ametujalia kufika wakati huu ambapo mwisho wa mwaka uko karibu. Tunaomba kwamba mwaka ujao utakuwa mwaka wa amani na wa mafanikio kwa Wakenya wote. Sisi viongozi ambao tunajua matatizo Wakenya wanapitia, hatutaki kuona tena Wakenya wakiumizwa ama wakiuawa. Nawaomba viongozi wenzangu kwamba tukienda katika likizo hii, tuzungumzie kuhusu amani na haswa kuhusu maendeleo wakati huu tunapoelekea manyumbani. Nawatakia Wakenya wote Krisimasi njema na mwaka mpya wa mafanikio haswa wale Wakenya wa Kaunti ya Taita Taveta, ambao walinipatia nafasi hii ya kuja Bunge hili la Kumi na Moja. Ahsante sana, Mhe. Spika."
}