GET /api/v0.1/hansard/entries/511379/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 511379,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/511379/?format=api",
    "text_counter": 519,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon.Chumel",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 318,
        "legal_name": "Samuel Chumel Moroto",
        "slug": "samuel-moroto"
    },
    "content": "wenzangu kwamba hata tukitengeneza karatasi nzuri namna gani, hakuna kitu ambacho kitafanyika. Lazima tuanze kusafisha nyumba ya wale ambao wanasimamia mambo ya usalama. Bwana Kimaiyo na Bwana ole Lenku wameumia kwa sababu wanatoka jamii ndogo. Wale wanaotoka katika jamii kubwa--- Mimi niko katika kamati ya usalama. Wakati mwingi hawa maafisa wakija katika mikutano yetu, huwa pana shida. Hii ni kwa sababu mkuu wa polisi anaweza kusema jambo lakini wale wenzake wawili wanakanyagia hilo jambo. Sharti tuanze kutengeneza mambo. Kwa sababu ya ukabila ambao umejaa katika Kenya hii, hakuna mahali tutafika. Wakati tutaanza kujadili vizuri suala hili kama nyumba nzima, lazima tuangalie vitu kama hivyo kuhakikisha kwamba hatufanyi mambo ambayo hayasaidii."
}