GET /api/v0.1/hansard/entries/512370/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 512370,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/512370/?format=api",
    "text_counter": 427,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Asante sana Naibu wa Spika kwa kunipatia hii nafasi ili name nichangie Hoja hii. Nashukuru mheshimiwa Musimba kwa kunipatia hii nafasi ijapokuwa napinga hii Hoja. Kwa ukweli sisi sote ni viongozi. Ni sisi tulimchagua huyu Spika. Sisi wenyewe inatupasa tujiheshimu kwanza kabla ya kwanza kumtaja Spika. Kufuatana na yale ambayo tumekuwa tukiona, sidhani tumeonyesha Wakenya heshima katika Bunge hili. Kile ambacho tumeonyesha ni kibaya. Tumejikosesha adabu sana. Tumeona wenzetu wakichukuwa chupa na kumwagia Naibu Spika maji usoni mwake. Kwa hivyo, sisi kama viongozi tujiheshimu kwa vile tumechaguliwa na wananchi ambao wanatuheshimu. Kuhusu hii Hoja, Mheshimiwa Musimba angechukua nafasi ya kukaa chini na kupendekeza Kamukunji ili tuwasiliane na tujadiliane kuhusu makosa tunayofanya humu Bungeni. Ukweli ni kwamba sisi tumefanya makosa makubwa sana na inabidi tuyarekebishe. Mimi ninapinga hii Hoja. Ninaopose hiyo kitu."
}