GET /api/v0.1/hansard/entries/513816/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 513816,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/513816/?format=api",
"text_counter": 162,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 128,
"legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
"slug": "richard-onyonka"
},
"content": "Ahsante sana, mhe. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja hii yenye makuu kwa nchi yetu. Kwanza, ningependa kusema kuwa nitakubaliana na Mwenyekiti wa Kamati yetu ya Bunge ya Ulinzi na Mashauri ya Nchi za Kigeni, mhe. Gethenji, ambaye amefafanua na kusema mengi kumhusu Meja-Jenerali Mstaafu Tumbo. Kwa kusema kweli, tuliketi na wanakamati wote tukazungumza na kujadiliana sana kuhusu ndugu huyo. Ningependa kusema kuwa, kama Kinara wa WalioWengi Bungeni mhe. Duale, nakubaliana kuwa ingekuwa vizuri iwapo waliosomea diplomasia wangekuwa na fursa ya kuitumikia nchi yetu katika Idara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni. Lakini tulipoangalia ujuzi wa huyu Bw. Tumbo, tuliitana na tukazungumzia mambo yake na kuelewana na kukubaliana kuwa ingekuwa vizuri kama Mheshimiwa Rais angepitisha jina lake ili awe balozi wa Kenya kule Somalia. Mhe. Spika, vile ndugu zetu wamezungumza katika Bunge hili letu leo ni kuwa Meja-Jenerali Mstaafu Bw. Tumbo ana ujuzi wa kimasomo, kikazi, kijeshi kwa kuwa ashasomea mambo ya kijeshi kule Pakistani na Marekani kwa shule kubwa kubwa za kijeshi na amefaulu na kusifika sana.Tukaangalia na kusema kwa kuwa Somalia ni nchi inayoendelea na vita mpaka sasa, pengine ingekuwa vizuri yeye aende pale ili ajaribu kujihusisha. Isitoshe, jambo tulilomuambia ni kuwa atajaribu kujihusisha na kuzungumzia pande zote kule Somalia ili tujaribu kupata nafuu na kuelewana na wao vile tungependa uhusiano kati ya Kenya na Somalia uwe. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}