GET /api/v0.1/hansard/entries/513817/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 513817,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/513817/?format=api",
    "text_counter": 163,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 128,
        "legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
        "slug": "richard-onyonka"
    },
    "content": "Ningependa kusema kuwa tuliuangalia uteuzi wake si kwa kikabila bali kama wengi walivyosema hapa, tungependa kusema kuwa tunakubaliana kuwa tungependa Mheshimiwa Rais Kenyatta ajumulishe Wakenya wote na ahakikishe kuwa tuna sura ya Kenya atakapokuwa anateua maafisa wa Serikali, hata kama ni mabalozi au viongozi wengine katika idara za Serikali. Hivyo ndivyo tunaweza kuendeleza nchi yetu ili iwe nchi inayoheshimika na kukubaliana na maadili ya kidemokrasia. Kumalizia, ningependa kusema kuwa ingawa Meja-Jenerali MstaafuTumbo alifanya kazi kwa Jeshi la Kenya, tunaamini kuwa akifika Somalia, atazungumzia masuala ya Somalia na Kenya na kumueleza Rais Kenyatta ukweli ulivyo. Tunaamini ataleta ujuzi wake wa kijeshi na kuzungumza na pande zote huko Somalia. Kama inawezekana, azungumze na kila mtu ambaye amejihusisha na mambo ya Somalia. Kwa hivyo, ningependa kusema kuwa na kubaliana na Hoja na vile Mwenyekiti wangu amesema, kuwa Meja-Jenerali Mstaafu Tumbo ni Mkenya halisi na aliye na ujuzi, tungependa kumuuliza mhe. Rais akubaliane na kuidhinisha uteuzi wake. Ahsante sana, mhe. Spika."
}