GET /api/v0.1/hansard/entries/513839/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 513839,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/513839/?format=api",
    "text_counter": 185,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Gichigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1909,
        "legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
        "slug": "samuel-kamunye-gichigi"
    },
    "content": "Ahsante, Mhe. Spika. Nilipokuwa nikija Bunge siku ya leo, nilikuwa nimejitayarisha kuipinga Hoja hii kwa sababu hivi majuzi, tuliletewa majina ya watu ili tuyakubali au tuyakatae, lakini tuliyakubali. Hayo yalikuwa majina ya walioteuliwa katika Tume ya Huduma ya Walimu. Siku ya leo, nilipoangalia Ripoti ambayo Kamati imetuletea, niliona kuwa Serikali imeleta jina la mtu ambaye amestaafu. Sisi wenyewe na hata Rais wetu na Naibu wake, tumekuwa tukiongea juu ya ukosefu wa kazi katika nchi hii. Zaidi ya asilimia 70 ya wale ambao wamekosa kazi ni vijana wetu. Kila wakati tunapoletewa majina ya watu ambao wamepatiwa kazi, ni watu ambao wamestaafu - wenye wamezidisha miaka 55 au 60. Nilipoongea na Mwenyekiti wa Kamati hii, niliambiwa kuwa wale ambao wamekuwa mabalozi katika Somalia miaka kadhaa iliyopita, wamekuwa wamekatalia hapa Nairobi kwa sababu ya kuogopa ukosefu wa usalama katika Mogadishu na nchi ya Somalia. Kwa sababu huyu Generali amekubali kuenda kutuwakilisha katika nchi ya Somalia, kukaa huko badala ya kukaa katika Jumba la National Social Security Fund (NSSF) hapa Nairobi, nitaunga mkono uteuzi huu. Tuko na shida sana katika nchi hii. Ningependa kumwambia Rais wetu, Naibu wake na Tume zote ambazo zitaleta majina ya watu ambao wameteuliwa ili wapitishwa na Bunge hili, kuwa tutapiga kampeni katika Bunge hili ikiwa watu hao hawatakuwa na miaka ya chini kidogo."
}