GET /api/v0.1/hansard/entries/513841/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 513841,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/513841/?format=api",
"text_counter": 187,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Gichigi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1909,
"legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
"slug": "samuel-kamunye-gichigi"
},
"content": "ikamkague mtu ambaye ameteuliwa kujiunga na JSC. Iwapo watatuletea watu ambao wamestaafu, nawaomba waheshimiwa tukatae. Jambo lingine ambalo ningependa kulitaja ni kwamba Kaunti yangu ya Nyandarua imesahaulika kabisa katika mambo ya uteuzi. Sisi hatuna mtu ambaye ameteuliwa kuwa Balozi ama Waziri. Pia, miongoni mwa Makatibu kwenye Wizara za Serikali, hakuna hata mmoja kutoka Kaunti ya Nyandarua ingawaje kuna wanaojihusisha tu na Kaunti hiyo. Kwa hivyo, ninamuomba Rais; anapoteua wafanyikazi wengine wakuu wa Serikali, aikumbuke Kaunti ya Nyandarua. Mhe. Spika, kuna shida kubwa kwenye mpaka wa nchi hii na Somalia. Kuna watu wanaofikiria kwamba magaidi wa Al Shabaab wanatushambulia kwa sababu tulipeleka majeshi yetu kule Somalia. Uhalifu unaofanyika katika Kaunti za Mandera, Garissa na Wajir umekusudiwa kuwafukuza wafanyikazi wa Serikali ambao wanazuia kuingizwa kwa bidhaa haramu humu nchini. Nilipokua kwenye Bodi ya KRA, tulijua kwamba ukosefu wa usalama katika mipaka yetu ulikuwa unasababishwa na watu wanaoingiza bidhaa haramu humu nchini. Lengo lao ni kuhakikisha kwamba hakuna maafisa wa polisi ama maafisa wa KRA ama maafisa wa Idara ya Uhamiaji kwenye miji ya mipakani. Kama kuna biashara ambayo inailetea Kenya hasara, ni ile ya kuingiza bidha humu nchini kupitia Somalia. Wengi miongoni mwetu hatutaki kuamini kwamba wanajeshi wetu walioko Somalia wanafanya biashara hiyo. Hatutaki kuamini kwamba hilo ndilo linalofanyika. Tunawaomba marafiki zetu wanaotoka kwenye kaunti hizo tushirikiane tuweze kuisaidia Serikali. Wafanyi biashara kutoka kaunti hizo, wakishirikiana na wengine ambao wako hapa Nairobi, wanafadhili makundi yanayohusika kwenye uhalifu unaochangia kutokuwepo kwa usalama. Ukiona Serikali imefikia kiwango cha kusema itajenga ukuta kati ya Kenya na Somali – jambo ambalo halistahili kufanyika kabisa – ni kwa sababu ya huo ukora. Mhe. Spika, kwa sababu Gen. Tumbo, ambaye ameteuliwa na Rais, amekubali kwenda Mogadishu, nitaiunga mkono Hoja hii. Lakini iwapo uteuzi wa baadaye hautazingatia sehemu zote za Kenya, na haswa Kaunti ya Nyandarua kukumbukwa, nitakuwa miongoni mwa Wabunge ambao wataupinga eteuzi huo. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii."
}