GET /api/v0.1/hansard/entries/514109/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 514109,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/514109/?format=api",
"text_counter": 100,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2715,
"legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
"slug": "esther-nyambura-gathogo"
},
"content": "ikifanya vibaya kwenye mitihani hakuna mtu atajua. Kuna shule ambazo hazina madarasa na mambo mengi ya kufaulisha shule. Tunayo hazina ya CDF. Sisi hapa tunaruhusiwa kusaidia shule kwa kutumia pesa za CDF. Kwa hivyo wale ambao wana shule ambazo hazina vifaa katika maeneo yao wanaweza kutumia pesa ya CDF. Kuna shule ambazo zinafanya vizuri lakini siyo lazima kila mtu aende kusomea huko. Muhimu ni kwamba tujue ni mbinu gani shule hizo zinatumia kupita mitihani. Tukikosa kufanya hivyo hali ya masomo itarudi chini. Wale wanaotia bidii watasikia vibaya kwa sababu ni vizuri kujulikana kuwa umefanya vizuri. Siku ile ulishinda uchaguzi, kama hungeambiwa wewe ndiwe mshindi ungesikiaje, Naibu Spika Wa Muda? Kwa hivyo, kwa heshima, ningeomba tuendelee kuorodhesha shule ili tujue ni shule gani zimeenda chini. Tusiseme eti shule fulani imeenda chini bali tujue palipo shida. Kuna shule tulisikia imefanya mtihani vibaya. Lakini shule hiyo ilipoangazwa kwenye runinga, tuliona zile shida ambazo watoto wanapitia. Wanafunzi wengine huenda kuchota maji na kwa hivyo hurudi shuleni wakiwa wamechoka. Inabidi tuwapatie maji ndiposa waache kwenda mtoni na wawe na muda wa kusoma. Nina hakika tukifanya hivyo watapita mtihani. Kwa hivyo, naunga mkono Hoja hii. Mimi ni mhubiri ijapokuwa sijateuliwa. Tuendelee kuombea hili Bunge."
}