GET /api/v0.1/hansard/entries/514110/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 514110,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/514110/?format=api",
"text_counter": 101,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadhegu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Ahsante Naibu Spika wa Muda, kwa fursa hii ambayo umenipa nami niweze kutoa maoni yangu kuhusu Hoja hii. Kwanza, naunga mkono Hoja hii kwa dhati. Ni jambo la kushangaza kuwa wenzangu wanasema ni vibaya kuorodhesha shule ama wanafunzi ambao wamehitimu vyema katika mitihani ya taifa. Tunaorodhesha shule ambazo zimefanya vyema ili umma upate kujua ni wapi matokeo yamekuwa mazuri. Watu watajiuliza ni kwa nini matokeo yamekuwa mazuri. Huenda ikawa ni kwa sababu ya vifaa vizuri vya shule, walimu, mazingara nakadhalika. Tusipoorodhesha shule na wanafunzi, ni lini umma utajua sehemu fulani inafanya vyema kuliko sehemu nyingine? Tusipofanya hivyo fedha za serikali zitapelekwa mahali fulani peke yake. Basi itakuwa rahisi kwamba ni sehemu fulani za nchi ambazo zitatoa vinara na wanafunzi shupavu. Si kwamba wao wamejaaliwa akili kuliko wenzao bali ni kwa sababu ya kuwa na vifaa bora. Mheshimiwa wa Rarieda ananiambia kwamba katika eneo lake kuna wanafunzi ambao hawana viatu. Anasema kwamba shule zao hazina mijengo wala maabara. Ingawa hivyo wamefanya vizuri. Walipata alama nzuri za “A”, “B” na “C”. Hii ni kwa sababu wanafunzi wenyewe wanaweza kusoma. Wanafunzi wanakosa vifaa vya kutosha. Tunaomba waorodheshwe ili watu wajue ni vipi wanafanya mitihani. Hata wabunge ambao wako Bungeni wameorodheshwa. Mbona sisi tukatae shule ziorodheshwe? Nakubaliana na wenzangu kuwa mara nyingi watu wamechukua nafasi hii ili kutengeneza hela katika zile shule zinazofanya vizuri kwa sababu ya kuorodheshwa. Serikali lazima ichukue jukumu la kuhakikisha kwamba tabia kama hiyo imekomeshwa. Tusiseme kwamba kwa sababu tabia hiyo ipo basi ni kwa sababu ya kuorodheshwa. Lazima shule ziwe na mpangilio. Sharti ziorodheshwe ndipo tutajua sehemu fulani inafanya vyema kwa sababu fulani na fulani. Nimesikia mwenzangu akisema kuna kamati ambazo zimeteuliwa kufanya utafiti na zimependekeza kwamba shule zisiorodheshwe. Mimi nafikiri hii ni kwa sababu Serikali imeshindwa kutekeleza majukumu yake hasa kwa kuhakikisha kwamba vifaa vya shule vimesambazwa nchini kote. Sharti Serikali ihakikishe kwamba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}