GET /api/v0.1/hansard/entries/514111/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 514111,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/514111/?format=api",
"text_counter": 102,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadhegu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "wanafunzi wanashindana katika mazingara ambayo ni sawia. Shule za hapa jijini Nairobi zina vifaa. Kwa hivyo walimu wanakimbilia huku. Wale waliobaki mashinani wana shida zao. Shule huko hazina vifaa. Kama Serikali itahakikisha imesambaza vifaa na walimu wazuri wanabaki mashinani, basi wanafunzi watakuwa wakishindana katika mazingara sawasawa. Kwa hivyo, naunga mkono Hoja hii. Nawasihi Wabunge wenzangu wafikirie ni nini wanachotaka kufanyia wanafunzi wetu wanaposema shule zisiorodheshwe. Juzi hatukupata hiyo orodha. Nini kimetokea? Orodha ziko. Hata katika kaunti yangu najua zile shule ambazo zimefanya vyema na zile ambazo hazikufanya vema. Nimejua upungufu uko wapi. Tunajua ni wapi tunatelezea. Hii ni kwa sababu shule zimeorodheshwa hata huko mashinani katika kaunti. Mnataka kuficha ukweli na hali tunaomba huo ukweli ujitokeze waziwazi ili tujue fedha zinapelekwa wapi. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja huu."
}