GET /api/v0.1/hansard/entries/514162/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 514162,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/514162/?format=api",
    "text_counter": 153,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadime",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "Ahsante sana, mhe. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Mwanzo kabisa ninaunga mkono hii Hoja ambayo imeletwa na mwenzetu, mhe. Njenga. Ukweli kabisa ni kwamba vijana wetu, haswa wale wa shule, wakati wako likizo huwa ni hatari sana kwa sababu hivi vijibwasha haviko tu mijini mikubwa ya Kenya bali viko katika kila sehemu ya Kenya. Ni tatizo kubwa na sugu kwa sababu mambo ya pombe na madawa, mihadarati ni hatari sana kwa vijana wetu. Hata Serikali hupoteza vijana wengi kwa sababu ya kutupatupa mikebe na vibwasha kila mahali."
}