GET /api/v0.1/hansard/entries/514164/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 514164,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/514164/?format=api",
"text_counter": 155,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadime",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": "Suala hili kwanza limeenea zaidi katika maeneo ya Kenya ambako hakuna kazi. Nikiangazia sana eneo Bunge la Mwatate, utakuta kwamba hatuna kiwanda hata kimoja. Mvua hakuna na maji ni tatizo. Tuko tu na wale ndovu wakubwa ambao wanakula chakula kingi na wanatumalizia chakula chetu shambani. Basi hao vijana, kwa sababu hawana shughuli nyingi, mambo ya pombe na madawa ndio hujishughulisha nayo. Ingekuwa ni vyema tutafute njia mwafaka ya kuwezesha haya mashirika angalau wadhibiti utupaji wa vitu hivi. Hata kile kiwango tumefikia kwa sasa hivi nchini, ingewezekana tungetengeneza mahala pia pa kuwezesha hawa vijana kutibiwa maanake wengine wako katika hali mbaya sana. Tungekuwa na rehabilitationcentres katika kila jimbo ingekuwa ni vyema zaidi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}