GET /api/v0.1/hansard/entries/514165/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 514165,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/514165/?format=api",
"text_counter": 156,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadime",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": "Nampa pongezi mhe. Njenga kwa kuleta hii Hoja maanake hili ni swala tata sana; vilevile ni swala ambalo linatutatiza sana sisi viongozi. Mambo ya pombe na madawa yako kila mahali Kenya nzima. Utawakuta watu hata mchana katika hali ya kujiburudisha ingawaje ni kujiharibu. Ingekuwa ni vyema kabisa hili swala lishughulikiwe kikamilifu na liwe ni kitu ambacho tumemalizana nacho. Vijana wetu ndio viongozi wetu wa miaka ijayo. Tukishughulikia hili swala itakuwa ni vizuri ."
}