GET /api/v0.1/hansard/entries/514184/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 514184,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/514184/?format=api",
    "text_counter": 175,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Chea",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1694,
        "legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
        "slug": "mwinga-gunga-chea"
    },
    "content": "haya. Kinachonivutia zaidi katika Hoja hii ni kwamba inapendekeza tuanzie mashinani. Hoja hii imezungumza hasa kuhusu watoto wetu wa shule. Hii ni ishara kwamba tunaenda kuambatana na yale wahenga walisema, kwamba ni lazima samaki tumkunje angali mbichi. Tunazungumza kuhusu masuala ya pombe, hasa pombe ambayo haijahalalishwa na sheria. Sijui kama mheshimiwa Kigo alikosea, lakini alisema kwamba pombe ya mnazi ni baadhi ya zile pombe haramu. Nataka kusawazisha maoni haya. Mnazi si haramu. Pombe hii inatoka kwenye mti aina ya mnazi na haina matatizo yoyote."
}