GET /api/v0.1/hansard/entries/514185/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 514185,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/514185/?format=api",
"text_counter": 176,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Chea",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1694,
"legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
"slug": "mwinga-gunga-chea"
},
"content": "Ningependa kusema kwamba unywaji pombe, hasa miongoni mwa vijana, umedidimiza uchumi sana. Vijana wanapoingilia unywaji pombe wanakosa kujihulisha na masuala ya maendeleo. Hivyo basi ni kweli kwamba kuna haja ya NACADA kujizatiti zaidi kwa kuibua mbinu mwafaka ambazo zitahakikisha suala hili linashughulikiwa vilivyo. Tatizo hili halihitaji tu suluhu kutoka kwa Serikali peke yake. Hili tatizo ambalo linatuhitaji sisi viongozi na wazazi kulitilia maanani. Hoja hii inazungumzia hasa matumizi ya pombe haramu katika miji yetu. Sharti tukubali kwamba jinsi tunavyoishi makwetu ni muhimu. Kwa mfano, si vema kuwatuma watoto wadogo dukani kununua pombe. Wazazi wakome kufanya hivyo. Sharti tuhakikishe tumewaonyesha watoto wetu mienendo mizuri."
}