GET /api/v0.1/hansard/entries/514980/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 514980,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/514980/?format=api",
"text_counter": 228,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kiungo cha muhimu sana katika serikali zetu za ugatuzi ni Bunge kule mashinani. Ni muhimu kusiwe na mapingano au mipaka katika utumiaji wa zile pesa kati ya Bunge zetu za ugatuzi. Nikisema hivi, natilia maanani ya kwamba hivi sasa tunavyozungumza, Kaunti ya Kilifi haiwezi kuwalipa wafanyakazi wake. Ni ukweli kabisa kwamba kuna shida huko mashinani. Kwa hivyo, ni muhimu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Biashara na Bajeti alete jibu kuhusu jambo hili Alhamisi hii inayokuja. Ni muhimu tupate jawabu maalum kesho ama kesho kutwa. Asante, Bw. Spika."
}