GET /api/v0.1/hansard/entries/515346/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 515346,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/515346/?format=api",
"text_counter": 209,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kisasa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13124,
"legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
"slug": "mshenga-mvita-kisasa"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Hoja hii imeniacha hoi kwa sababu mwamba ngoma huvutia kwake. Je, ni kweli dada Sen. (Dr.) Zani kama Mpwani anataka tuiunge Hoja hii mkono? Kama Wapwani tuna nini? Mimi nikiwa na uwezo ndio ningefanya choyo niseme kila mtu ale chake. Je, tulipofika sasa baada ya miaka 50 kutoka tupate Uhuru, tunasema kila mtu ale chake? Naipinga Hoja hii kwa sababu mimi mwenyewe nilianzia shule ya chekechea mashambani. Nikaenda shule mjini ya secondari na chuo kikuu. Nilijiunga na Aga Khan nikiwa mtu mzima. Bw. Spika wa Muda, labda dada Sen. (Dr.) Zani anaongea kwa niaba ya Nairobi lakini kama ni kwa niaba ya Wakwale ama Wapwani yeyote, bado hatujafika kiwango ambacho unataka kutupeleka. Binadamu yeyote akitoka nje hata akienda kwa jirani akirudi nyumbani, mawazo yatakuwa tofauti. Tumeangalia safari ambazo tunaenda na tunashukuru sana Seneti kwa sababu kila tukienda katika nchi hizo tunarudi kama tumesoma vitu tofauti. Je, hizi shule zikifanywa za county sisi tukipata C-tutafika wapi? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}