GET /api/v0.1/hansard/entries/515348/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 515348,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/515348/?format=api",
    "text_counter": 211,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mimi ningekuwa na uwezo ndio ningesema kila mtu ale chake lakini kwa sasa naona bado tunahitaji watu kujumuika. Tunahitaji watoto wetu kuchanganyika na watoto wengine. Shule nzuri ni nini? Shule nzuri ni wanafunzi kuwa na nidhamu, waalimu kuwepo na madarasa kuwa mazuri. Sisi kama Wapwani tuna nini ili tuseme kwamba tutapata alama kama wenzetu? Kaunti yetu ina nini kwa sasa ambayo tutajifanya kwamba tumebobea ili kuwa chetu kiwe chetu? Tunahitaji waalimu wetu na watoto wetu wachanganyike National Assembly wengine kwenye Kaunti zingine. Tunahitaji Kenya yetu iwe kitu moja. Kwa hivyo, iweje kwamba elimu ambapo mtoto anaenda kujifunza iwe kwamba anajua lugha yake pekee yake? Kuna watu ambao hawajatoka nje ya Pwani. Kuna mtu anaishi Kilifi na hajafika hata Mariakani au Mombasa. Tunashuru Mwenyezi Mungu kwa sababu hii ni kama dua ya kuku labda kwa mwenzangu dada Sen. (Dr.) Zani lakini kama Wapwani tunahitaji kaunti zingine. Inafaa tuwe taifa moja. Sisi Wapwani tunahitaji watoto wetu pia wafike Migori ili waweze pia kuongea lugha ya huko. Tunahitaji watoto wetu pia waongee lugha ya kitende. Tunahitaji watoto wetu waende Bonde la Ufa ili waweze pia kuongea Kikalenjin. Bw. Spika wa Muda, kama nilivyosema hapo awali, mtaniacha hoi kwa sababu mkiniangalia sina ile fursa ya kupiga kura. Sijui itakuwaje? Wakati huu tuna shule za chekechea. Tulivyosema, tuna darasa moja muhimu kwenye kila shule. Kama vile tulivyoweka darasa muhimu kwenye chekechea tutakuwa na darasa muhimu kwenye shule ya msingi ili watoto wote waende pamoja. Tunahitaji pia shule ya sekondari tukiangalia nini ambacho hatuna. Kwa mfano, hatuna bweni ama mahabara ya utafiti. Bw. Spika wa Muda, vile nilivyosema hapo awali, tunataka watoto wetu wachanganyike, wajumuika na kutabaruka na watoto wengine nchini Kenya. Lakini tukisema kwamba mimi nimekuja kuishi Nairobi kwa hivyo wale ambao tumewawacha Pwani, tuwasahau na tuseme kwamba kila shule ambayo ni ya kitaifa, basi ibaki hivyo. Ni ombi langu kwamba kama shule itaitwa shule ya Serikali, iwe na vifaa ambavyo vinatakikana kutoka chekechea hadi sekondari. Kwa hivyo, ikiwa shule ni ya Serikali, itabulike kama shule ya kitaifa. Bw. Spika wa Muda, nina mengi ya kusema lakini ninasihi Hoja hii isipitishwe kama vile ilivyo kwa sababu Wapwani hatuna cha kujivunia wala hatujui tutaanzia wapi. Kuna watoto ambao hata viatu hawana na wamejaa na funza. Shule ina vumbi na kila mtu anasoma kwa kutazama. Wakati huu hata mtu akijifanya kwamba amepata shahada ya digrii ama ni profesa bado tunasoma. Kuna mambo mengine ambayo mtu hawezi kuyajui yote kwa sababu binadamu hapewi kila kitu. Pengine mtu atapewa akili lakini mwendo wake hautakuwa wa kufaa. Bado tunajifunza kama Wakenya. Miaka hamsini imepita baada ya Uhuru lakini bado tunahitaji kutoka nje. Bw. Spika wa Muda, tunahitaji watoto kusoma katika shule za chekechea zilizo karibu na nyumbani. Mtoto anapojiunga na shule ya msingi anafaa kuenda Mombasa, shule ya sekondari aende Nairobi au Kirinyaga hata kama wanafunzi wa kule wataongea lugha ya kabila yao. Anaweza hata kwenda katika shule ya Maranda ili watu wa Maranda pia wajivunie kuwa na mtoto kutoka Mkoa wa Pwani. Tukisema kila mtu asomee shule ya kwao, hilo halitakuwa wazo nzuri. Saa hizi tunajaribu kuwa jamii moja. Migogoro tuliyonayo labda ni kwa sababu kila mtu anajiita kwao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}