GET /api/v0.1/hansard/entries/515361/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 515361,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/515361/?format=api",
    "text_counter": 224,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kisasa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13124,
        "legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
        "slug": "mshenga-mvita-kisasa"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Nafikiri atakuwa na wakati wa kunikosoa kwa sababu hapo mbeleni, Sen. Kagwe alikuwa akitaka sekta ya elimu igatuliwe. Kwa hivyo, siko mbali na Hoja aliyotoa. Sidhani kama nimeteleza. Unikosoe kama nimeteleza. Nilikuwa tu najaribu kutetea. Mambo yaliyo katika Hoja hii yakigatuliwa itakuwa vipi? Wacha nimalize hapo kwa sababu naona kama nakosea. Hata hivyo, wapwani hatujafikia kile kiwango cha wenzetu. Hatujafikia kima cha shule za upili za Alliance na Maranda. Kwenye gazeti la leo, mwanafunzi wa kwanza katika shule moja huko Kwale alipata Gredi C-. Wale waliopata Gredi E, ambayo yaitwa reki, ni 37. Huo ndio wasiwasi wangu. Kwa hayo machache, ninapinga Hoja hii."
}