GET /api/v0.1/hansard/entries/517182/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 517182,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/517182/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kisasa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13124,
"legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
"slug": "mshenga-mvita-kisasa"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa muda zaidi ili niendelee na kuchangia Mswada huu ambao tunataka kupitisha. Maana ya harambee ni kujumuika, kutabaruku na kuvuta pamoja. Tukiangalia tutaona ya kwamba huwezi kusema kama kitu si kizuri ama hakifuatwi vile ipasavyo, kitupiliwe mbali. Harambee zinatujenga sana. Nimefanya utafiti na watu wangu kule vijijini na wakanipasha ya kwamba, wao wanaenda kwa harambee, kwa sababu kadha wa kadha.Kwa mfano,malipo ya hospitali hayaepukiki. Sio kila mmoja wetu ana ule uwezo, kibali fulani ama analipiwa na shirika fulani. Hapo ndio watu wangu hutafuta harambee. Lakini tukiangalia mbali na yale malipo ya hospitali, utaona ya kwamba pia kuna malipo mengine ambayo yanahitajika. Kwa mfano, mtu akifa, itabidi kuwe na malipo ya kuhifadhi maiti. Je, watu wangu watafanyaje? Itawabidi wafupishe ule muda wa maiti kukaa katika hifadhi maiti, kwa sababu kile kibali ambacho chatolewa na polisi kwa muda wa kuomboleza labda ni cha wiki moja peke yake. Bw. Naibu Spika, tunapotunga sheria, tusisahau kuwa pia, sheria ni msumeno. Hivi juzi, sisi hapa kwenye Seneti, tulikkukmbwa na msiba, na harambee ilitusaidia. Hivi mnavyotuona, tunang’ara lakini ilibidi pia tutumie harambee. Mmoja wetu alituaga na The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}