GET /api/v0.1/hansard/entries/517186/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 517186,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/517186/?format=api",
"text_counter": 206,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Tukiangalia pia shule, watu wangu wanafuata harambee kwa sababu ya karo ya shule. Tukiangalia kitita hiki cha Constituencies Development Fund (CDF), hakitutoshelezi. Kila mtu atakuwa akipewa pesa ambazo zinatakikana kule shuleni. Utaona ya kwamba wakati mwingine shule inataka Kshs50,000 lakini mtoto amepewa Kshs5,000. Je, ile Kshs45,000 itatoka wapi? Lazima tuangalie. Mimi naomba sana kwa dhati kuwa Wakenya tuishi pamoja, tuvute pamoja na tusaidiane mpaka wakati ule ambapo tutakuwa tumejinasua. Bw. Spika wa Muda, tukiangalia pia huu mradi wa Mama wa Taifa, Margaret Kenyatta, hiyo pia ni harambee. Je, mwajua kuwa pia ile ni harambee? Harambee sio pesa peke yake. Harambee pia ni zawadi fulani kama vile yeye ametutunuku vile visanduku vya mobile clinics . Harambee ina mahali pake katika nchi hii, na tukiangalia Harambee, ni jadi yetu. Hakuna mazishi ya mtu mmoja wala harusi ya mtu mmoja. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba harambee imekuwa ni kama jambo la kulazimishwa kwa sababu utakuta jina lako kama kiongozi katika kadi ya mwaliko kama mgeni wa heshima bila kujulishwa. Imekuwa kama ni njia fulani ya sisi viongozi kuoneshana ubabi wa kisiasa. Utakuta nikichanga, kwa mfano, Kshs5,000 sipewi heshima kama yule kiongozi ambaye atachanga Kshs20,000 ama Kshs50,000. Kwa hivyo, sisi wenyewe kwa wenyewe ni kama tunaonyeshana ubabe. Inafaa tujiangalie sisi wenyewe kwa sababu tutafilishishwa. Utakuta mtu fulani amefiwa na mamake mara tano. Ni nani ambaye ana mama watano? Kwa hivyo sijui nikubali harambee iendelee ama isiendelee. Lakini ikikomesdwa, sijui watu wangu watafanyaje. Siwezi kusema kwamba iendelee kwa sababu sisi kama Maseneta hatuna mfuko wote wa hela na kwa hivyo unapofika pale inabidi ujikunje kwa sababu vidole vyote si sawa. Kwa hivyo, inafaa tuweke mikakati fulani ambayo itawasaidia watu wetu. Bw. Spika wa Muda, kama kule ninakotoka, tunahitaji harambee zaidi. Na ukienda kule bara, inahitajika zaidi. Wenzetu kutoka bara ndio mababe wa harambee kwa sababu wakiitana kwenye mchango wa mazishi ama harusi wanachanga kima cha pesa ambacho kinastaajabisha. Sisi Wapwani, mara nyingi jamvi latosha kwenye mazishi. Lakini ningependa kusema kwamba harambee bado ina mahali pake kwenye jamii zetu. Mwanzilishi wa taifa aliona kwamba hatutaweza kuishi bila kusaidiana kwa sababu kama manvojua, upweke ni uvundo. Ni lazima kila mtu awe na marafiki ambao atasaidiana nao kwa sababu huwezi kuwa mazishini peke yako. Ama utapika pilau kwenye harusi na ule peke yako? Kwa hivyo hii ni harambee. Hata kuenda kula ama kutabaruk na wengine ni harambee. Si lazima utoe, upande gari na uende zako. Kwa hivyo harambee itazidi kusaidia watu wetu kwa sababu kuna vitu vingi ambavyo ni lazima watu wengi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}