GET /api/v0.1/hansard/entries/517188/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 517188,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/517188/?format=api",
"text_counter": 208,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "wasaidiane ili wanufaike. Je bila harambee Kenya tutaenda wapi? Nimejiuliza swala hili wikendi nzima. Kwa hivyo inafaa mikakati kabambe iwekwe kwa sababu unyonge umetuzidi. Tunaambiwa kwamba Seneti ni Jumba kuu lakini ni kivipi kama mfuko hauna kitu? Mkono mtupu haulambwi. Hasa ukienda mazishini na huna chochote, utajiona mnyonge kwa sababu hutatajwa kuleta chochote. Ukiangalia wenzetu wa Bunge la Kitaifa, wao wana hazina ya CDF na wamechukua fursa hii kuonyesha ubabe katika hizi harambee. Mara nyingi mheshimiwa akionekana, bajeti hubadilika; hata kama wangeketi kwenye jamvi, itabidi kuwe na madoido fulani. Kwa hivyo harambee hizi wakati mwingine zinatutatiza. Lakini hatuzipingi kwa sababu kama nilivyosema hapo awali, hakuna mtu ambaye hahitaji harambee. Mara kwa mara sisi wenyewe kwa wenyewe tunachangiana hapa. Lakini uzuri wetu hapa ni kwamba tunaweka kima fulani. Hatuonyeshani ubabe katika Seneti, na ninawashukuru wenzangu. Ninaunga mkono Mswada huu lakini itabidi tuweke mikakati fulani."
}