GET /api/v0.1/hansard/entries/518403/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 518403,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/518403/?format=api",
"text_counter": 300,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kisasa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13124,
"legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
"slug": "mshenga-mvita-kisasa"
},
"content": "Asante sana Bw. Spika wa Muda. Kusema kweli, kichwa kimeniuma mchana mzima. Mimi ninatoka katika Kaunti ya Kilifi na sipingi sheria hii. Lakini hata mtoto pia akizaliwa, atanyonyeshwa halafu utaangalia njia zingine za kumpa chakula kabla ya kuamua kuwa hautamnyonyesha tena. Tukiangalia wanyama vile vile, utaona kwamba hakuna mzazi anayemuacha mtoto wake mara moja. Nilivyosema kuwa natoka Kilifi, ni kwamba sisi huko hatuwezi kuishi bila ya harambee. Sipingi Hoja hii, lakini lazima tuangalie njia nyingine mbadala za kuwasaidia watu wetu kwenye sheria hii. Je, kutakuwa na hazina fulani ambayo wale ambao wako kwenye kaunti ambazo ziko chini kimaendeleo na ambazo zina udhaifu au unyonge wa fedha watafaidika nao? Bw. Spika wa Muda, ninaona Sen. (Dr.) Khalwale ameinamisha kichwa chake chini, lakini ninamwambia kwamba akiwa daktari, Kilifi, ataletewa vitelevisheni ambavyo vyote saa hizi vingekuwa vimezimwa; vitu ambavyo ni duni. Watu hawana hata hati miliki za ardhi za kuwawezesha kuziweka rehani na kusema kwamba “muache mgonjwa wangu akae hapa halafu kesho nitaleta pesa.” Hivyo basi, utajaziwa vitarakilishi na vyombo vyengine vya nyumbani ambavyo hivi sasa vingekuwa vimezimwa ilhali wewe kama daktari hata haujui utaviuza wapi kwa sababu hauwezi kuvichukua uvipekele mahali ili upate pesa ndio hospitali yako iendelee. Bw. Spika wa Muda, hii ni sheria ya maana sana, lakini tukiangalia kwa makini, tumefundishwa vibaya kama Wakenya kuanzia zama za muanzilishi wa Taifa hili; hayati Mzee Jomo Kenyatta. Harambee ni moyo ambao umetufunza ya kuwa hakuna arusi wala matanga ya mtu mmoja. Ni lazima kijiji kizima kishiriki katika mambo haya. Lakini tukiangalia katika mkono wangu wa kushoto, utaona kuwa watu sasa wanajifanya hawajiwezi kabisa. Ukiangalia mazingira watu wanayofanyia kazi, utakuta kuwa lazima mtu atadanganya kuwa leo nimefiwa na babangu, mwaka ujao tena atasahau aseme amefiwa tena na babake, ilhali mwaka mwingine atasema amefiwa na babake tena. Sasa, utashangaa kuwa mtu huyu ana baba wangapi. Hapa tukiangalia, tutaona kwamba shida hii inayoitwa h arambee, lazima kuwe na hazina fulani ambayo itaenda kule rizavu kuwasaidia wale wasiojiweza. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}