GET /api/v0.1/hansard/entries/518405/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 518405,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/518405/?format=api",
    "text_counter": 302,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, twachangia watu ambao walikufa miaka mingi sana iliyopita, lakini utajuaje kwamba unaambiwa ukweli ama unadanganywa? Kwa mfano, ukienda matangani, Sen. (Prof.) Lesan ataenda huko, atatoa Kshs20,000 na hautaambiwa kuwa hizi fedha zipo. Sen. Kisasa naye akienda huko matangani, naye pia atatoa Kshs20,000 na hawatajali iwapo mimi ni Seneta aliyechaguliwa ama niliyeteuliwa. Sen. Wetangula naye pia akienda huko, atatoa Kshs20,000. Matanga yamekuwa ghali sana, na ukienda huko, hawatakwambia kuwa Seneta huyu ama yule ametoa pesa kiasi fulani. Kwa hivyo, kuna shida kubwa sana kwa sababu Wakenya tumezoea uwongo mwingi na tumezoea kujirudisha chini. Hata ukiangalia arusi zetu, zinakuwa za kifahari hadi unashangaa yote haya ni ya kazi gani. Utaona pia katika matanga, mtu yuazikwa kana kwamba atatembea; yuavishwa viatu vya Kshs20,000. Kwa hivyo, tuko na shida kubwa. Kama vile wenzangu walivyosema hapo awali, utakuta ya kwamba ukionekana tu umefika, basi hii pesa ya matanga itabidi iongezwe na makadirio yake lazima yawe makubwa na yasiyoeleweka kabisa. Ndio maana nikasema kuwa Mswada huu umeniumiza roho sana kwa sababu sijui kama nitauunga mkono au nitaupinga. Lakini nikiukataa pia, itabidi labda watu wazikwe kama wanavyozikwa Waislamu; ukifa leo, basi, uzikwe leo leo. Hii ni mila yetu, hivyo basi, hatuwezi kusema “yatosha; hatutaki tena kusaidiana.” Je, tukisema Harambee zifungiwe milango, tutaenda wapi sisi Wanakilifi ambao tumezoea kusaidiana? Bw. Spika wa Muda, Harambee ni za kutokea jadi; je, hii jadi tutaikata vipi? Je, hii jadi tutaisemaje kuwa leo ni mwisho? Je, tutatafuta njia nyingine mbadala ya hii"
}