GET /api/v0.1/hansard/entries/518501/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 518501,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/518501/?format=api",
    "text_counter": 92,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Bule",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1029,
        "legal_name": "Ali Abdi Bule",
        "slug": "ali-abdi-bule"
    },
    "content": "Bw. Spika ninakushukuru kwa kunipatia nafasi hii nikiwa na masikitiko makubwa sana, kwa sababu huu ni wakati Wakenya wengi wanaomboleza ufisadi uliokithiri nchini. Wakenya wengi wameathirika kwa mikono ya viongozi ambao hawajali hali ya wanyonge. Wakenya walituchagua kuambatana na sheria na kutupatia uwezo wa kuwakilisha kaunti zetu. Kufuatana na Kipengee 96(1) na (2) tumepewa uwezo wa kuwawakilisha, kuwalinda, kuwatumikia, kuwatatea na kuunda sheria zinazoweza kuleta maendeleo nchini Kenya. Hatukuchaguliwa kukaa hapa Bungeni na kusindikiza wafisadi na wakora. Bw. Spika inafaa hii Seneti ipeana mwongozo kwa Wakenya. Inafaa tume maalum ibuniwe ili ichunguze kiwango ambacho ufisadi umeathiri nchi ya Kenya. Asilimia 99 ya Wakenya wanakufa njaa, hawana makazi na ni walala hoi. Kenya hii ilichagua Rais na Makamu wa Rais---"
}