GET /api/v0.1/hansard/entries/521077/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 521077,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/521077/?format=api",
"text_counter": 131,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Gichigi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1909,
"legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
"slug": "samuel-kamunye-gichigi"
},
"content": "matatizo ili kazi iendelee vizuri. Pia waende washughulikie walimu wakuu ambao wanakataa kutii amri ya Wizara kuhusu karo. Vile wanakataa, ni kama hizo pesa zinaenda kwa mifuko ya watu. Ni afadhali wangekuwa wakiambia Serikali iweze kusaidia mahali ambapo pana upungufu wa pesa badala ya waendelee kuumiza wazazi na wanafunzi kwa kuitisha karo ya juu zaidi. Ijapokuwa naunga mkono, ningetaka kutaja maneno kadha. Kwanza, kuna shida kidogo kuhusu hawa maafisa ambao wameteuliwa hapa. Tutapitisha Hoja hii na nitaiunga mkono kwa sababu ya wakati na wamehitimu kuchukua nafasi hizo. Lakini ukiangalia wale wote ambao wameteuliwa, vile Serikali yetu ya Jubilee na Manifesto yake na pia vile Katiba inasema, hakuna kijana hata mmoja ambaye amepewa nafasi. Ukiangalia wale wameteuliwa, mmoja ni miaka 60, mwingine ni miaka 59, mwingine ni miaka 56 na mwingine ni miaka 62. Sisemi wazee wasifanye kazi, lakini ni muhimu pia vijana wa kati ya miaka 30 na 40 wapewe nafasi. Wengi wa walimu ambao wanasimamiwa na hii Tume ni vijana. Kila wakati wakienda kutafuta msaada kwa Tume, wanaenda kwa wazee watupu. Hata wale ambao wako kule kwa wakati huu pamoja na Katibu wote miaka yao imesonga. Ni kweli tunataka ile hekima, lakini vijana pia wapewe nafasi kwa uteuzi ambao utakuja. Naona kuna umuhimu tubadilishe sera ya elimu ambayo inasema kitambo mtu ateuliwe katika Tume hiyo, anastahili kuwa amefanya kazi zaidi ya miaka kumi. Mwalimu akitoka chuo kikuu akiwa na miaka 25 na umpatie miaka 10, atafikisha miaka 35. Kwa hivyo, ni muhimu sana vijana wapewe nafasi. Kwa Serikali yetu na hata Rais wetu, ningetaka hili jambo la vijana liangaliwe kwa sababu litaleta shida katika hii nchi. Jambo lingine ni kuwa hawa wote ambao wameteuliwa ni walimu ambao wamefanya kazi wakakuwa maafisa wakubwa katika idara mbali mbali. Kwa kweli, hii ni Tume ya walimu. Lakini ni makosa Tume yote inasimamiwa na walimu. Wanahitaji pia taaluma zingine kama vile sheria na uhasibu. Vile wako, itakuwa ni kama shule itakuwa ikiendelea katika Tume hii. Nikimalizia, ni muhimu pia tuangalie mambo ya tume kama hizi. Ni kweli wana uwezo wa kikatiba, lakini wote wakumbuke kuwa wako katika Serikali. Vile tume za kikatiba zimekuwa zikifanya ni kukaa kando na kusema zisiambiwe kwa sababu zina uhuru na zitafanya vile zipendavyo. Lakini kila mwisho wa mwaka, wanakuja kwa Serikali Kuu kuomba fedha za kugharamiaa bajeti zao. Ni muhimu sana waweze kujua kwamba lazima wafanye kazi na idara zingine za Serikali na tume zingine. Tuko katika Serikali moja. Zote tuko katika basi moja ya kuelekea kuleta maendeleo katika nchi hii yetu. Nashukuru sana, Mheshimiwa Spika."
}