GET /api/v0.1/hansard/entries/523040/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 523040,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/523040/?format=api",
    "text_counter": 222,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwakulegwa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 101,
        "legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
        "slug": "danson-mwazo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Hoja hii ni ya maana sana. Ningependa kumshukuru Seneta wa Makueni, jirani yangu, kwa kuleta Hoja hii mbele ya Seneti hii. Bw. Spika wa Muda, miaka mitano baada ya kupata Katiba na miaka miwili yetu kuwa hapa katika Seneti, imekuwa vyema Hoja hii kuletwa hapa ili tuizungumzie. Serikali za ugatuzi zimekuwa na shida kubwa. Shida hizo zimekuwa kwa sababu pesa zinazopewa sehemu za ugatuzi zimegawanyishwa kutumia vigezo kulingana na idadi ya watu, maeneo na mambo mengine. Kwa hivyo, shida ambayo tumekuwa nayo ni kwamba zaidi ya nusu ya maeneo ya kaunti yanazozana kuhusu mipaka. Mipaka hiyo imekuwepo tangu siku za ukoloni lakini ilianza kubadilishwa mwaka wa 1962. Mipaka ilipobadilishwa mwaka wa 1962, viongozi waliokuwa mamlakani, walianza kuongeza sehemu zao. Hiyo ndiyo sababu unasikia watu wakilalamika kuhusu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}