GET /api/v0.1/hansard/entries/523042/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 523042,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/523042/?format=api",
    "text_counter": 224,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "mipaka ya kaunti za Isiolo, Meru, Taita- Taveta, Kwale na Makueni. Zaidi ya nusu wanagombana kwa sababu waliokuwa katika mamlaka wakati huo na waliokuwa na nafasi walianza kujiongezea nafasi za utawala. Walianza kuwasukuma wale waliokuwa wanyonge. Kamati ya kuangalia maeneo ya Bunge hayakuzingatia ugatuzi bali wilaya katika nchi hii. Wananchi walitaka mipaka ya maeneo mbalimbali ibadilishwe, lakini haingeweza kubadilishwa. Kufikia mwaka wa 1992, mipaka ya wilaya yalibadilishwa. Mipaka hiyo ndio tunayoitumia kugawa maeneo ya ugatuzi. Baada ya miaka 51 ya Uhuru na miaka minne tangu kupata Katiba mpya, wakati umefika kwa Bunge la Seneti kupewa nafasi yake. Bunge la Seneti ndilo lenye uwezo wa kuiangalia mipaka ya kaunti na wala si Bunge la Kitaifa. Kwa kuangalia mambo haya hatutaki kutumia vyombo vya kisasa lakini hekima kubwa. Tumesikia kwamba jamii mbalimbali wamegawanywa na mipaka. Wale ambao ni wachache katika kaunti fulani wanasema wanaonewa kimaendeleo. Utaona ya kwamba watu fulani katika kaunti wananyimwa fedha za maendeleo kwa sababu ni wachache. Bw. Spika wa Muda, tunaomba pia ndugu zetu wa Bunge la Kitaifa watupe nafasi hii vile tumewapa nafasi yao. Wao ndio wanaofanya mgao wa pesa za nchi hii. Tunawaomba pia Wabunge wa Bunge la Kitaifa watupe nafasi kama vile tumewapa nafasi. Wao ndio wanafanya mgao wa pesa za nchi hii na sisi ndio tumepewa nafasi na Katiba ya kugawanya maeneo ya ugatuzi. Wakati wa kubadilisha sheria umefika."
}