GET /api/v0.1/hansard/entries/523044/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 523044,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/523044/?format=api",
    "text_counter": 226,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bi. Spika wa Muda, tunafaa tuwe na kamati mpya itakayosimamia mipaka na shughuli zote za uchaguzi. Tunataka kuwa na kamati ambayo tutaipiga msasa kama Seneti. Tunawahimiza watu ambao watasimamia kamati hiyo watumie vyombo fulani ili kutoa uamuzi ambao utaponya vidonda ambavyo vimekuwa kwa miaka 51. Tunafaa kuangalia ni kwa nini mambo haya yamezidi. Hii ni kwa sababu tunatumia mbinu za kisasa kama idadi ya watu, maeneo na kadhalika. Hii ndiyo sababu mambo yamezidi. Mambo hayo ndio yanayotumika kugawa pesa. Kama mambo hayo ndio yanayotumika kugawa pesa, utapata Kaunti ya Taita Taveta inazozana na ndugu wao wa Kaunti za Makueni, Kwale na Kajiado. Tumesukumwa pande zote na tunataka mambo haya yaeleweke. Shida si kwa sababu ya madini, kodi, na kadhalika. Kuna mambo mengi ambayo watu wa kaunti wanataka yasuluhishwe. Kwa mfano, katika kaunti yangu, kuna jamii ya Wataita kule Mackinnon. Wameishi hapo lakini wanatawaliwa na Kwale. Katika ugavi wa pesa za maendeleo, kunaweza kuwa na uonevu. Kuna watu ambao wanabaguliwa na watoto wao hawapati pesa za basari. Mada hii imekuja wakati mzuri kuponyesha vidonda sugu ambavyo vimekuwa katika nchi ya Kenya. Kuponyesha vidonda hivyo, hatutaviangalia vyombo vya digitali. Bi. Spika wa Muda, tukiangalia historia yetu, tutajua watu walikuwa wapi na nini kilichokuwa wapi. Mambo haya yatakuwa na uchungu lakini tunafaa kukubali The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}