GET /api/v0.1/hansard/entries/523046/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 523046,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/523046/?format=api",
    "text_counter": 228,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kuyarekebisha mara moja. Kumekuwa na maeneo ambayo yamekuwa na maonevu ya Serikali kwa upande wa maendeleo. Katika maeneo hayo, si pesa tu za maendeleo ambazo hazikupatikana. Mipaka ya maeneo hayo iliwekwa kiholela. Hawakuwa na viongozi wakati huo. Sasa wana viongozi katika Seneti hili ili haki itendeke. Wakati umefika kwa sheria hiyo kubadilishwa ili tuyatatue matatizo tuliyo nayo sasa. Tukichelewa, matatizo yataendelea kuzidi. Ningependa kama Seneta wa Taita Taveta katika Katiba hii mpya, niyatatue mambo ya mipaka. Ningependa kuyatatua mambo ya maendeleo na mambo ya ugawaji wa pesa kulingana na idadi ya watu na maeneo ili ukweli na haki utendeke. Kumekuwa na tetezi vile tunavyosoma katika magazeti. Naomba pia waandishi wa magazeti wasije wakaanza kusema kwmaba watu hawa wataondolewa hapa na kupelekwa mahali pale. Haya yote yataongeza uhasama na kuleta vita. Kile tunaomba kama Bunge la Seneti ni kwamba sheria iwekwe. Tunafaa kuwa na nafasi yetu ya kuweka kamati ambayo itabuni mbinu na sheria za kuyatatua matatizo haya. Bi. Spika wa Muda, bila kuyatatua matatizo katika kaunti zetu, magavana watazidi kuzozana. Wakizidi kuzozana, mambo ya maendeleo katika nchi yetu yataharibika kwa sababu watakuwa wakiangalia ni nani atakayeichukua sehemu hii ama ile. Watu wengi hapa huwa wakiyaangalia maeneo Bunge. Tunafaa kuyatatua mambo haya tukiwa na hekima kubwa na kwa kutumia vyombo vya kisasa na maarifa. Tunafaa kuangalia historia ya Kenya ili watu wa Kisumu na Maseno wasije wakagawanywa na mipaka na kuanza kupigana. Tunafaa kutumia wakati huu ili tutatue matatizo hayo. Tunafaa kuleta mapenzi zaidi, uelewano na maendeleo. Bi. Spika wa Muda, ninahakika Hoja hii itaungwa mkono na wengi wetu. Tunafaa kuiweka kamati kwa sababu wengi wameonewa kwa sababu hawawezi kujitetea mahali walipo. Pengine ni wachache ama haki zao za kisiasa zimeonewa maana wao ni wachache. Ninahakika tutaunda kamati ambayo itatatua matatizo mengi na kuleta usawa, ukweli na ugatuzi utaendelea. Kwa hayo machache, ninaunga mkono kwa dhati Hoja hii kwa sababu imekuja kwa wakati unaofaa. Tukiwa hapa, kama maseneta wa kwanza, tuwe na hekima, maarifa na nia ili tuyatatue matatizo haya kwa sasa na kwa vizazi vijavyo."
}