GET /api/v0.1/hansard/entries/524929/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 524929,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/524929/?format=api",
"text_counter": 258,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "kuwa ni muhimu kuwa na mkaguzi wa hesabu, kwani itawezesha Serikali kutumia fedha kwa njia ya sawa sawa, na njia ambayo itakuwa ya kujulikana. Inatakikana pia kuona kuwa mkaguzi wa hesabu hataegemea upande wowote katika kufanya kazi yake. Inatakikana kazi yake kubwa kuona kuwa anakagua hesabu za fedha, ama rasilimali za pesa za wananchi na kuona kuwa hesabu hizo ni sawa sawa. Katika kipengele cha 25 cha Mswada huu, ningependa kuunga mkono kwani nimeona kimependekeza kuundwa kwa bodi ya ushauri, ambayo itakuwa ikimshauri mkaguzi wa hesabu katika kufanya maamuzi. Vilevile, naona kuwa katika Mswada huu, kazi ya bodi hii imeweza kuonyeshwa katika kipengele cha 27, na kazi yake kubwa itakuwa kutoa ushauri kwa mkaguzi wa hesabu ili kuona kazi hii itafanyika sawasawa. Ni lazima pia ofisi ya mkaguzi wa hesabu ipewe uwezo wa kuchukua hatua kwa wafujaji wa rasilimali kwa sababu tumeona kuwa ofisi hii ya mkaguzi wa hesabu hutoa hesabu zake na ikasema watu kadhaa, ama kitengo fulani, wamefuja mali ama rasilimali. Haya yamekuwa ni maoni tu yametolewa na hakuna hatua yoyote imechukuliwa. Kwa hivyo, ningependa kuona kuwa ofisi hii imepewa nguvu pamoja na bodi yake wakati wowote ambao itaona kuna ufujaji was pesa, ama hesabu hazikuenda sawa sawa ichukulie hatua watu ambao watakuwa wamefanya mambo yasiyo ya sawa."
}